Pages

Ads 468x60px

Labels

Thursday, August 1, 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND AONDOKA BONGO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand kwa maafisa waandamizi mbalimbali wa serikali wakati wa kumsindikiza mgeni huyo aliyehitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini mchana huu. Hapo akipeana mkono na Mkumbwa Ally wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa


Akisalimiana na Dr Laurent Ndumbaro


Akisalimiana na Dr Hamisi Mwinyimvua


Akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Omar Mjenga


Akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki


Akiagana na Kamanda wa Mkoa maalumu wa kipolisi wa Dar es salaam Suleiman Kova.PICHA NA IKULU.



Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dar es salaam wakipunga mkono kumuaga rasmi Waziri mkuu wa Thailand leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri mkuu wa Thailand Bi.Yingluck Shinawatra katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (katikati) . Bi. Shinawatra amemaliza ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment