Pages

Ads 468x60px

Labels

Sunday, August 25, 2013

MDOGO WAKE MAREHEMU STEVEN KANUMBA, AIBUKIA DSM NA KUSEMA MANENO MAZITO.


Lameck Charles Kanumba anavyoonekana kwa karibu, baada ya kuzungumza mengi.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.
MDOGO wake marehemu Steven Charles Kanumba, anayeitwa Lameck Charles Kanumba, ameibukia jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa kaka yake anamtokea ndot
oni na kuzungumza naye mambo mengi, yanayohusu familia na sanaa ya Tanzania.

Lameck aliyasema hayo mapema leo mchana, ikiwa ni miezi mine tangu alipokuja jijini Dar es Salaam kwenye kumbukumbu ya kaka yake, ambapo pia historia inafanana kutokana na baba yao kuendelea kula kona na kuacha kuwatunza watoto wake na kuwatelekeza kwa mama zao.
Charles mdogo wake Kanumba anavyoonekana pichani
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Lameck alisema kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam, ambapo pia anatumia nafasi hiyo kuhangaikia masuala ya sanaa ambayo yapo kwenye damu yake.

Marehemu Steven Kanumba.
 
Alisema hawajawahi kuonana uso uso kwa Kanumba, kutokana na yeye kuishi mkoani Mbeya na mama yake, wakati siku anakufa alishindwa kupata nauli ya kuja kwenye mazishi yake.

“Naendelea kuumia kutokana na kufariki kwa kaka kabla ya kuzungumza naye uso kwa uso, lakini pia inashangaza kwakuwa mara kadhaa huwa ananijia ndotoni na kuzungumza naye hasa mambo yanayohusu familia.

“Baba hajanihudumia tangu mtoto kama ilivyokuwa kwa kaka Kanumba, hivyo bado naona nina mengi ya kufanya kwa ajili ya kumuenzi marehemu aliyeifanyia mambo mema Tanzania kwa kupitia sanaa,” alisema.

Aidha, Lameck yupo katika maandalizi kabambe ya kuandaa filamu yake inayojulikana kwa jina la ‘Charles’, huku akiishi kwa msamaria mwema, anayelikana kwa jina la Fatuma au mama Kenge, mtaa wa Sinza Uzuri, jijini Dar es Salaam.

Friday, August 2, 2013

5 things to watch out for under Mourinho’s new look Chelsea.


Updated: August 1, 2013



José Mourinho, a name that is bound to raise eyebrows and send shivers down the spines of the opponent. Called “the special one” and rightly so after what he has achieved, it’s time for Mourinho’s second inning at Chelsea.

With Sir Alex Ferguson leaving behind a legacy, the stage is all set and here are the 5 things to watch out for under Jose Mourinho’s Chelsea.

John Terry’s role:

Captain, leader and legend . With Mourinho confirming that John Terry will continue to serve as the captain, there is a little doubt in everybody’s mind if Terry still has what it takes to lead the Blues.

With the age catching up on the 32 year old and the new duo of Cahill and Luiz establishing themselves as a formidable Centre back partnership, it might just be the season when Terry is shown the bench more often than not.

The Future Of MAZACAR:

Having played just one full season together the trio of Mata, Hazard and Oscar, commonly known as “MAZACAR”, have transformed the way the blues play football. When employed together they form a devastating force, enough to rip apart any team by the scruff of its neck.

While being prolific at attacking, the defensive side of the trio is something to be worked on. They have been slow to react to counter attacks and lack the ability to read the game in their own half. It is up to the coach to decide if the “MAZACAR” can be tweaked in a way that helps maintain the balance of the side or whether it is time to look at other options like André Schurrle or Kevin De Bruyne.

Role of The Youth:

Ever since Roman Abramovich took over at Chelsea, the blues have made huge progressive strides towards the development of their academy players. The Cobham has been completely revamped to produce world-class academy youth products. But the Chelsea management has been blamed on numerous occasions for letting these young prodigies leave and then turn into potential stars of this beautiful game.

Mourinho is known for delivering success in the short term, with the help of a couple of signings. It would be interesting to see if the young blues actually get some minutes under their belt or it would be the old guards who will continue to run the show.

Relationship with the British media:

10th June 2013, Mourinho’s first press conference as a Chelsea manager once again, with 250+ reporters. “Not sure how many managers would draw this kind of crowd. Love him or loathe him, the man has charisma” said Ollie Holt from the Mirror. Jose Mourinho is known for his expressive remarks. Be it calling himself “Special One” or comparing the players with eggs.

A favorite amongst the media , Jose knows how to deal with them and uses this to his advantage. The battle between the British media and Jose is something to really look forward to.

Fernando Torres:

Ever since the 50 mil pound man joined from Liverpool, a Chelsea article is not complete without the mention of a certain Spaniard, Fernando Torres. From being a goal machine to terrorizing opponents with his pace, it would be easy to say that Fernando Torres was one of the most feared strikers of his times. Little did he know about how his life would change after his arrival at Chelsea.

Already labeled as a flop and rightly so because of his horrendous spell at Chelsea, netting a total of just 34 goals in 131 appearances for the blues. His career seems all but finished, adding to that is the revival of the young and flamboyant Lukaku and a possible transfer of Wayne Rooney. There seems to be a glimmer of hope, keeping in mind his great form in Europa League which helped Chelsea get the only silverware of the season, and registering themselves in the history books for holding both the Champions League and Europa League at the same time. To add to this, his run continued in Confederations Cup where he managed another golden boot.Maybe the winds of fortune are turning in the favor of El Niño, maybe Jose can get the best out of the Spaniard and make him the man we shelled out 50mil for. For all the Chelsea fans and for Torres the first 6 months are pivotal to decide his destiny in the blue colors.

All eyes are set on Jose now, with the promise of the upcoming season to be one of the most interesting one’s. And Chelsea already being touted as the favorites just tops it all up.

Thursday, August 1, 2013

WAZIRI MKUU WA TANZANIA ASHITAKIWA RASMI....MAWAKILI 19 WAJITOA MHANGA


Kituo cha Sheria na Utetezi wa Haki za Binadamu (LHRC) na Chama Cha Wanasheria Tanzanyika vimefungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, vikiomba mahakama hiyo itoe tafsiri za kisheria katika baadhi ya Ibara.

Kesi hiyo ya Kikatiba ambayo imepewa namba 24 ya mwaka huu, na ambayo bado haijapangiwa jaji, wadaiwa ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taasisi hizo ambazo zinatetewa na mawakili wa kujitegemea Harold Sungusia, Francis Stolla na wengine 17, kwa mujibu wa hati yao ya madai, walalamikaji hao wamewasilisha jumla ya maombi mawili ambayo wanaomba mahakama itoe tafsiri ya kisheria katika Ibara hizo kwa kuwa wamewasilisha kesi hiyo ya Kikatiba chini ya sehemu ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo
inaainisha Haki na Wajibu Muhimu.
Wakili Sungusia alilitaja ombi la kwanza kuwa, wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa majadiliano kwa wabunge wawapo ndani ya bunge ambayo inasomeka hivi: “kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katikaMahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.”

Wakili Sungusia anadai kuwa Ibara hiyo ina ubaguzi ndani yake kwani inayoa uhuru kwa mbunge kujadili ndani ya bunge na wakati anajadili jambo hata kama amevunja haki za mtu mwingine hataweza kushitakiwa wala kuhojiwa jambo ambalo anadai linakinzana na Ibara ya 13(2) ya Katiba ambapo Ibara hii inasomeka hivi; “ Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake’.

‘...sisi tunaomba mahakama itamke wazi kuwa Ibara ya 100(1) inakwenda kinyume na matakwa ya Ibara 13(2). Zinakinzana, kwa kuwa ibara ya 100(1) ya Katiba inatoa haki tu kwa upande wa mmoja wa wabunge uhuru wao kutohojiwa na inawanyima haki ya kuwahoji au kuwashitakiwa wabunge wanaotoa kauli zao bungeni hata kama kauli hizo za wabunge zimevunja haki za wananchi,”alidai wakili Sungusia.
Wakili Sungusia alilitaja dai la pili kuwa ni kuiomba mahakama hiyo itamke kuwa kauli ya Waziri Mku, Pinda ambayo ililitaka Jeshi la Polisi kuwapiga wale wote wanaokiuka amri za jeshi hilo, kama kauli hiyo nayo inalindwa na kinga iliyowekwa katika Ibara ya Ibara ya 100(2) ya Katiba ya nchi ambayo inasomeka hivi: ‘Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.’

Katiba mkutano wa bunge uliomalizika hivi karibuni , Waziri Mkuu Pinda akiwa ndani ya bunge aliliagiza jeshi la polisi kuwapiga wale wote wanaokaidi amri za jeshi hilo, kwasababu serikali imeshachoshwa na vitendo vya baadhi ya wananchi wanaokaidi kwa makusudi amri za jeshi la polisi , kauli iliyoleta mhemko kwa jamii huku wengine wakiipinga utekelezaji wa agizo hilo na wengine wakiunga mkono, hali iliyosababisha LHRC hivi karibuni ilizungumza na waandishi wa habari wakimtaka Pinda afute kauli yake hiyo ama sivyo watamfikisha mahakamani.

Source; Itv Tanzania

BREAKING NEWS: JOSEPH AKISAINI MKATABA WA KUICHEZEA SIMBA SC


MLIMA KILIMANJARO 'KUSHNEY', BARAFU YOTE YAYEYUKA.



Taswira ya Mlima Kilimanjaro inavyoonekana kwa sasa baada ya kuyeyuka Barafu yote, ikiwa imebakia sehemu kidogo tu juu ya Kilele cha Mlima huo, ni kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi na uhalibifu wa Mazingira uliokithiri.

Taswira ya mlima huo na Kilele cha Mlima Kibo

Mlima Kilimanjaro Kushney, kama unavyoonekana ukiwa hauna Barafu huku iliyobaki ikielekea kumalizika kwa kuyeyuka.
 
CHANZO: SUFIANI MAFOTO

WATOTO KUMENYANA NDANI YA TOTO PARTY, IDDI MOSI ART GALLERY MBEZI BEACH, DAR



Kampuni ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.


Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.


Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.

Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

WAZIRI MKUU WA THAILAND AONDOKA BONGO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand kwa maafisa waandamizi mbalimbali wa serikali wakati wa kumsindikiza mgeni huyo aliyehitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini mchana huu. Hapo akipeana mkono na Mkumbwa Ally wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa


Akisalimiana na Dr Laurent Ndumbaro


Akisalimiana na Dr Hamisi Mwinyimvua


Akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Omar Mjenga


Akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki


Akiagana na Kamanda wa Mkoa maalumu wa kipolisi wa Dar es salaam Suleiman Kova.PICHA NA IKULU.



Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dar es salaam wakipunga mkono kumuaga rasmi Waziri mkuu wa Thailand leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri mkuu wa Thailand Bi.Yingluck Shinawatra katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (katikati) . Bi. Shinawatra amemaliza ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.

ANGALIA PICHA ZA MSHILIKI WA BIGBROTHER ALIYETOLEWA NANDO AKIWA CLOUDS FM


Mshiriki aliyetolewa Big Brother 2013 "The Chase" Jumapili iliyopita Amm Nando akiwa na Mussa Hussein (katikati) na Wasiwasi Mwabulambo kwenye Jahazi Jumatano 31 Julai 2013.PICHA ZOTE NA CLOUDS FM





Ammy Nando akiwa na Mtayarishaji wa kipindi cha Jahazi la Clouds FM Emmanuel Likuda.