Pages

Ads 468x60px

Labels

Saturday, May 20, 2017

HADITHI YA SUNGURA NA SIMBA

HADITHI YA SIMBA NA SUNGURA Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kutambua taabiko lake na kumtunuku chakula pasi na haja ya kukitolea jasho. Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye… Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea Ayala mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye uwanda wa nyasi fupi. Simba alimwacha Sungura na akakurupuka kumkimbiza yule Ayala. Vishindo kelele na purukushani za Simba na Ayala vilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini. Baada ya kumkimbiza Ayala kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura. Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, “ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi.”

Saturday, May 6, 2017

WANAFUNZI 32 WAFARIKI HAPOHAPO

.O.M.G MUNGU AWAREHEMU WOTE MLOPATA MISIBA Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo including(joint examinations), taarifa zinasema wamebaki watoto(3) tu wengine wamefariki, shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium school UPDATE: Coaster inasadikiwa kuwa na zaidi ya abiria 30 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio :Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi >UPDATES:Ni watoto watatu (3) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasiwasi vifo vikaongezeka >UPDATES:Gari lilikuwa na zaidi ya abiria 30 wanafunzi 25,waalimu (4) wote wa kiume na dereva >UPDATES:Kati ya majeruhi watoto watatu(3) wawili wako mahututi kabisa na mmoja amepasuka kichwa >UPDATES:Maajabu ya ajali hakuna damu zozote zilizotapakaa licha ya watu wengi sana kufa! >UPDATES:Majeruhi mmoja kati ya( 3) amefariki kabla ya kufikishwa hospitali,kwa hiyo taarifa zinasema wamebaki majeruhi wawili walioko ICU >UPDATES:Kuna mkanganyiko mwingi kuhusu chanzo cha ajali ila nature ya eneo la ajali ni mteremko mkali na kuna daraja,ni eneo ambalo dereva anatakiwa kuwa makini kabisa,kwa dareva asiyemwangalifu inaweza tokea lolote,hebu angalia hapo gari lilipotumbukia na haikuwa ina over take ,u can diagnose the nature of an Mwonekano wa gari kwa mbele baada ya kupata ajali. MORE UPDATES: UPDATES: Maiti 32 zimepokelewa katika Hospital ya Lutheran Karatu, miongoni ni walimu 2, dereva 1 na wanafunzi 29, wavulana wakiwa 11 na wasichana 18 waliokuwa wanasoma Lucky Vincent Nursery and primary school. -Mola awatie nguvu wazazi na wafiwa wote kwa ujumla. Endelea kufuatilia=> http://bit.ly/2pfWLoJ Source Jamiiforums